Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akipongezwa na mchungaji Canon Chamwenye wa kanisa Anglikana Msingisi mara baada ya kumaliza kuongea na akina mama juu ya kuanzisha kiwanda ili waweze kujikwamua katika maisha yao.
Mmoja ya akinamama akitoa shukrani ya kuku kwa mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe afanikisha ushawishi wa ujenzi wa viwanda kwa kuanzia na wanawake kanisa la Anglikana Dinari ya Rubeho Gairo. Ushawishi huo ulianza mwezi wa sita mwaka 2017 ambapo Mhe. Mchembe alihudhuria mkutano wa wanawake wa kanisa hilo akiwa Mgeni Rasmi. 

 Katika mkutano huo Mhe. Mchembe aliwashawishi akinamama hao kupitia umoja wao waanzishe kiwanda ili kiwainue kiuchumi. Aidha wapate mahali pa kuuza mbegu za alizeti ambazo kwa sasa alizeti ni kati ya mazao makuu ya biashara wilayani Gairo. 

 Hatimaye mpango umekamilika na Mhe. Mchembe amechangia pesa za Kitanzania shilingi laki tano kuhamasisha ujenzi wa kiwanda. Jumla ya gharama ya mradi ni shilingi milioni kumi na tisa. Majengo yanaendelea kufunguliwa na mradi unategemewa kuanza mwishoni mwa mwaka 2018. Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wana Dinari hiyo iliyojumuisha Kata ya Rubeho na Msingisi. Wanawake ni nguzo ya Maendeleo na uchumi wa viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...