NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la kitegauchumi mkoani Dodoma.

Kilichomfanya Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa 12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Aprili 23, 2018.

“Ninyi mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” 

Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 

Rais pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.“Nimefurahi kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania, ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira wakati wa ujenzi.” Alipongeza. 
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.
Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...