Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Mipango Miji Mijini na Vijijini kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa John Lupala amesema Serikali imejipanga vema kuhakikisha miji mikuu nchini inakuwa katika mpangilio unaotakiwa huku akifafanua ipo haja ya kushirikisha sekta binafsi katika kufanikisha mkakati huo.

Prof.Lupala ametoa kauli hiyo jana  jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau mbalimbali katika mkutano wa majadiliano wa namna inayoweza kufanikisha mkakati wa Serikali kupitia Wizara hiyo kufanikisha kupangilia miji mikuu yote nchini huku akielezea pia mkakati wa miaka 10 uliopo ambao utahusisha kupima , kupanga na kumilikisha.

Akizungumza zaidi kuhusu ambavyo wamejipanga kuhakikisha miji mikuu inakuwa katika mpangilio unaotakiwa amesema kuna mikakati mbalimbali ya kufanikisha mchakato huo ambapo upo wa miaka mitano na ule wa miaka 10.

Amesema kwa kushirikiana na wadau ambao wanahusika na masuala ya mipango miji wanaamini wataharakisha kuweka mpangilio mzuri wa miji ili wananchi sasa waweze kufuata, tofauti na siku za nyuma ambapo wananchi walikuwa wanatangulia kuanzisha mji halafu namna ya kuupangilia mji 
unachelewa.

Amesema mkakati wa kufanikisha mpangilio wa miji ni wa kitaifa ingawa kuna baadhi ya maeneo tayari wamekamilisha kupanga mji na kuongeza wataendelea kufanya hivyo katika maeneo yote.Profesa Lupala amesema anatambua kuna changamoto ya wananchi kutokuwa na uwezo wa kujenga kulingana na namna ambavyo wizara inataka lakini ifahamike kuwa wamejipana vema kuhakikisha kunakuwa na miji ambayo itakuwa imepangika.

"Niseme tu kama wizara tumejipanga vilivyo na katika kipindi hiki cha miaka mitano lazima tuwe na Master plan' ambayo sasa itatuongoza na ukishakuwa nayo inakuwa rahisi kushirikisha wadau kuangalia namna ya kuiharakisha."Kuna kampuni zaidi ya 60 za upimaji na upangaji na tunaamini tukiwashirikisha tutakwenda kwa kasi zaidi.Ifahamike Master Plan haindaliwi na Wizara bali ni kazi ya halmashauri ni kazi yetu ni kuratibu,"amesema.

Amesema programu ambazo zinaandaliwa ni za muda mrefu na lengo lake ni kuona miji mikuu yote ya mikoa inakuwa na master plan na inapokuwepo ni rahisi kuandaa michoro.Alipoulizwa ni miji gani ambayo haipo kwenye mpangilio mzuri, Profesa Lupala amejibu kuwa ipo miji mingi tu ambayo haiko kwenye mpangilio na miongoni mwao lipo Jiji la Dar es Salaam ambalo linaongoza kwa kutokuwa kwenye mpangilio mzuri na kuongeza pia Mwanza,Dodoma na Arusha.

Hivyo wanaendelea na kazi ya kuweka miji hiyo kwenye mpangilio unaoeleweka na kufafanua katika mpango wa miaka 10 wa kupanga, kupima na kumilikisha wananchi watakuwa wakichangia gharama za upimaji maeneo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...