Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limekutana na wajumbe wanaounda baraza hilo kwa lengo la kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa ya sheria mpya ya vyama vya siasa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda amesema katika kujadili mapendekezo mjadala utaanzia katika kamati ya Baraza vyama vya siasa ‘Kamati ya sheria na Utawala Bora’ inaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Hassan Almas na Makamu Mwenyekiti, Sudd Said Sudd.
Alifafanua kuwa Kamati ya Sheria na utawala bora itapokea mpango kitita katoka katika mawazo ya wanachama wa baraza hilo na kuongeza kuwa mchakato wa kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa haujatendeka pamoja mchakato wa mapendekezo ya sheria usajili wa vyama vya siasa.
Shibuda amesema baraza hilo liko huru bila kusukwa na mtu yeoyote.Amesema ndani ya wiki mbili inatakiwa kamati ya sheria na utawala bora iwe imekamilisha na baada ya hapo wiki mbili zingine iwe ni kwenda kamati ya baraza la vyama siasa inayoongozwa na Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda (pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cho cha baraza la vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakifatilia ajenda katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...