Meli hizo ni: Kaluba yenye usajili namba IMO 6828753 iliyokamatwa tarehe 27 Desemba 2017 ikiwa na wastani wa kilo 1,600 za dawa za kulevya huko katika maeneo ya Jamhuri ya Dominican Republic; na Andromeda yenye namba za usajili IMO 7614666 iliyokamatwa kwa kusafirisha silaha kinyume na Sheria za kimataifa. Meli zote mbili zimesajiliwa Tanzania kupitia taasisi yetu ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar ambayo ndiyo imepewa mamlaka ya kusajili meli za nje.
Hapa kwetu Tanzania tuna aina mbili za kusajili Meli; usajili wa Meli zenye asili ya Tanzania na zile zenye asili ya Nje. kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali, siku zote tumekuwa tunaheshimu na kutekeleza kikamilifu majukumu yetu ya kimataifa yaliyowekwa kupitia mikataba na maazimio mbalimbali ya vyombo hivyo
Ndugu Waandishi wa Habari, kwa mujibu wa mkataba wa UNCLOS 1982 kila nchi imepewa haki ya kufanya usajili wa meli kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa na sheria za nchi husika.Kwa upande wa Tanzania, usajili wa meli za kimataifa unasimamiwa na Sheria Na 5 ya mwaka 2006,

(Kwa upande wa SUMATRA ina Merchant Shipping Act ya mwaka 2003. Sheria hi inaruhusu usajili wa meli inayomilikiwa na Mtanzania, au meli inayomilikiwa kwa ubia kati ya Mtanzania na raia wa nchi nyingine. Kwa sheria hii ili meli ipate usajili wa SUMATRA na kuruhusiwa kupeperusha bendera ya Tanzania ni lazima umiliki wa meli uhusishwe na raia wa Tanzania kwa umiliki wote au kwa ubia lakini ni lazima Mtanzania awe na hisa nyingi. 
Vilevile kampuni hiyo ya umiliki lazima iwe ya Kitanzania kwa maana ya kusajiliwa na kujiendesha kutokea Tanzania hata kama kampuni hiyo inamilikiwa na watu wasio Watanzania. Na kwa upande wa Zanzibar kupitia ZMA wana Maritime Transport Act ya mwaka 2006).
Ndugu Waandishi wa Habari, nimewaita hapa kuzungumza nanyi na kupitia kwenu kuzungumza na wananchi wenzangu kuhusu taaarifa ya kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha zikiwa zinapeperusha bendera ya nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...