Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii .


SHIRIKA la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO), limeamua kugharamia matibabu kwa wananchi ambao wamepata majeraha mwilini kutokana na mlipuko wa moto ambao umetokana na kutoboka kwa bomba la gesi uliotokea maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, ambapo kwa sasa majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Ofisa Habari wa Dawasco Everlasting Lyaro amesema wameamua kugharamia matibabu ya majeruhi hao baada ya kujiridhisha ni kweli wamepata majeraha kutokana na mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi.

Amesema kuwa wafanyakazi wa Dawasco wakiwa katika eneo hilo la Buguruni wakiendelea na shughuli zao za kuziba bomba la maji la nchi 10, kwa bahati mbaya wakatoboa bomba la gesi na kusababisha moto kuanza kuwaka na kuleta madhara kwa baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo. 

"Watu ambao wamepata majeraha kutokona na mlipuko huo wa moto uliotokea Buguruni ni watatu.Hivyo tumefika Hospitali ya Taifa Muhimbil kwa ajili ya kuwasalimia na kuwapa pole na kubwa zaidi ni kugharamia matibabu yao wakiwa hospitalini hapo,"amesema.

Mmoja wa wakazi wa eneo la Buguruni jijini Mariam Rubaa ambaye watoto wake wawili wamepata majeraha kutokana na kuungua moto amesema anaishukuru Dawasco kwa msaada huo wa matibabu kwa waliojeruhiwa na kuongeza kilichotokea ni ajali kwani hakuna aliyetarajia kama moto ungetokea eneo hilo na kusababisha madhara kwa wananchi. 
 Mmoja wa wahanga wa mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi akiwa kwenye gari la wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kupatiwa matibabu

Mmoja wa wahanga wa mlipuko wa moto ambao ulitokana na kutobolewa kwa bomba la gesi akishushwa kwenye gari la wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kupatiwa matibabu. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...