KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.

Vijana kutoka Chuo Cha Munister nchini Ujerumani, leo wametembelea Kituo cha Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo Kigamboni Dar es Salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira.

Vijana hao zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani na baadaye kushiriki katika mafunzo ya ushonaji nguo kwenye mradi wa ushonaji nguo wa kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazokabili vijana na kinamama.

Kituo hicho cha Taasisi ya TaDEDO hadi sasa kina vijana 83 ambao kwa namna mojawapo walikosa fursa ikiwemo ya kutoendelea na masomo ambao sasa wanapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa kubuni na kushona nguo ambapo baadhi yao tayari ni mafundi.
Vijana wa Kituo cha ubunivu na ushonaji nguo cha Taasisi ya Kijamii ya TaGEDO, wakimwelekeza jinsi ya kutumia cherehani, kijana Astrid Naundorf kutoka Chuo Kikuu Cha Munister, wakati vijana wa Chuo hicho walipotembelea Kituo hicho, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) Venance Kalumanga akichoma taka, wakati yeye na wenzake wa Taasisi hiyo, walipoungana na Vijana kutoka Chuo Cha Munister nchini Ujerumani, kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni, dar es Salaam, leo
Vijana wa TaGEDO wakishirikiana na Vijana hao kutoka Ujerumani kukusanya taka wakati wakifanya usafi kwenye ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam, leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...