TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara. 

 Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo. 

 Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara ambao uliandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...