Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (kulia) kutokana na nchi yake kuisaidia Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo madaktari, wauguzi na kutoa matibabu kwa watoto. Katikati ni Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi na matibabu kwa watoto.
Mwanamuziki kutoka nchini Israel Maestro Nir Brand akiwaimbia wimbo watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati balozi wa nchi hiyo Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Taasisi hiyo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. 
Baadhi ya watoto wanaotiba katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan alipokuwa akiwaaga wakati wa ziara yake aliyoifanya jana katika Taasisi hiyo. Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart (SACH) imegharamia matibabu ya watoto 40 tangu Novemba 2015 hadi sasa ambao walitibiwa nchini humo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...