Na Lydia Churi, Mahakama, Songea

Mahakama ya Tanzania itashirikiana na Wadau wake ili kuhakikisha inawajibika ipasavyo na kufikika kirahisi ili wananchi wapate haki kwa wakati.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma jana, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali alisema Mahakama haitaweza kufanya kazi ya kutoa haki bila kushirikisha wadau wake.

Alisema Mahakama kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano hivi sasa iko kwenye Mpango maalum wa kumaliza kesi zote za zamani ambapo awamu ya kwanza ya Mpango huo iliyoanza mwezi Aprili, itamalizika leo Mei, 26.

Alisema ili kumaliza kesi hizo wadau wa Mahakama ni muhimu kwa kuwa wataharakisha na kurahisisha utendaji wa shughuli za Mahakama .

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Songea, Mhe. Wambali amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kuachana na vitendo vya rushwa na lugha mbaya kwa wananchi wanaofika mahakamani kutafuta haki zao.

Alisema kwa kufanya hivyo taswira ya Mahakama kwa jamii itakuwa ni chanya na Mahakama kuendelea kuwa kimbilio la wengi.

Jaji Kiongozi ameanza ziara katika Mahakama Kuu, Kanda ya Songea na Mtwara yenye lengo la kukagua shughuli za Mahakama na kusisitiza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama (2015-2020).

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Binilith Mahenge amesema endapo Mahakama itatekeleza kwa vitendo nguzo tatu za Mpango Mkakati wake ni dhahiri kuwa dhana ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...