NA VICTOR MASANGU, KIBITI

UONGOZI wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani imeanza kutekeleza maagizo yaliyotolewa Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ya kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya hususan katika maeneo ya Delta kwa kununua vifaa tiba, madawa, pamoja na vitanda maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakinamama wajawazito.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika mahojiano maalumu kuhusina na utekelezaji wa maagizo hayo ya naibu Waziri Mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo alisema kuwa kwa sasa tayari wameshaanza kununua vifaa mbali mbali katika zahanati  ili kuweza kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaokwenda kupatiwa matibabu.

Alvera alisema kwamba hapo awali katika sekta ya afya hasa kwa upande wa wananchi waliokuwa wanaishi  maeneo ya visiwani (Delta) walikuwa wanakabiliwa na changamoto  ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa kipindi kirefu kutoka na sehemu zenyewe ufikaji wake kuwa ni  mgumu kutokana na kutumia usafiri wa majini.

“ Ni kweli hivi karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya katika Wilaya yetu mpya ya Kibiti, na kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kujionea changamoto zinazowakabii wananchi,hivyo alituagiza sisi kama watendaji tujipange na kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo,hasa katika sekta ya afya na kimsingi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kununua mambo muhimu ambayo yanahitajika kwa wananchi wetu,”alisema Mkurugenzi huyo.

Alibainisha kuwa licha ya Wilaya hiyo ya Kibiti kuwa ni mpya lakini uongozi wa halmashauri hiyo wameshaanza kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wao katika maeneo mbali mbai ikiwemo  sekta ya afya, elimu, miundombinu pamoja na maji  ili kuweza kuwasogezea huduma kwa ukaribu.

Pia Mkurugenzi huyo alisema moja ya jitihada ambazo wamekwisha zifanya ni pamoja na kupeleka nishati ya umeme wa Solar power katika zahanati ya Salale,kupeleka kitanda maalumu kwa ajii ya kujifungulia kinamama wajawazito katika zahanati ya Mchinga ikiwa sambamba na kupeleka Solar Power nyingine katika zahanati ya Mfisini.

Kadhalika alisema nia na madhumuni yao makubwa ni kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Naibu waziri hasa kwa kuwaangalia zaidi wananchi wa maeneo ya vijijini na wale wanaoshi sehemu za Delta katika kuwafikishia huduma mabli mbali wanazostahili.


HIVI karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya mpya ya Kibiti na ambapo aliweza kubaini kuwepo kwa changamoto mbali mbali katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu, usafiri, hivyo aliagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuweza kuzitatua haraka iwezekanavyo  ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleo bila ya kuwa na vikwazo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa sambamba na kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kulia akizungumza na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua shughuli za kimaendeleo pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...