SERIKALI imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. 
Mheshimwa Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.

 'Natoa agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.' 

Akiwa katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.
Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo.Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi. Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri.Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri. Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri. HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...