MKUU wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa (pichani) ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.

 Akiwa ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.

 Akihitimisha taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu Mkurugenzi, Mhandisi Kweka.

 “Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa  Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani. Lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa. Ofisi hizi mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.

 “Niishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.

 Mkuu huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo ya fremu za madawati badala ya madawati.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinazoonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Bw. Yohana Sintoo.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Bw. Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...