Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kulia) akielekea katika Gati namba moja la Bandari ya Tanga kuangalia shughuli mbalimbali zinazoendelea bandarini hapo. Penmbeni yake ni Mhandisi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi.

Na Adili Mhina, Tanga.
Mamlaka ya Bandari nchini imeshauriwa kuangalia taratibu za kurasimisha bandari bubu ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazopitishwa katika maeneo hayo zinakubalika kisheria. 

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati  timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tahmnini ya shughuli zinazotekelezwa bandarini hapo. 

Mwanri alieleza umuhimu wa kurasimisha bandari bubu baada ya kupata taarifa kuwa katika Mkoa wa Tanga pekee kuna bandari bubu takriban 42 ambazo zinaendesha shughuli mbalimbali bila  ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari. 
Mhandisi wa Bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi (mwenye t-shirt) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (koti jekundu) juu ya kina cha maji katika bandari hiyo. Upande wa kulia ni Bw. Jordan Matonya na Bi Anna Kimwela, wachumi kutoka Tume ya Mipango. Upande wa kushoto (mwenye miwani ya jua) ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bibi Moshi Mtambalike.

Mwanri alieleza kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho suala hilo kwani licha ya Serikali kupoteza mapato yake wapo baadhi ya watu wanaotumia njia hizo nyakati za usiku kuendesha shughuli zinazoenda kinyume na kisheria na taratibu za nchi, hivyo kuchochea uhalifu.

“Kuna umuhimu mkubwa kuangalia shughuli zinazoendelea katika bandari bubu kwa kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanaopaswa kulipa kodi wanatumia maeneo hayo kupitisha bidhaa bila kulipa kodi na wengine wanatumia bandari bubu kuendesha biashara haramu. Ni lazima kuanza kufanya utaratibu wa kurasimisha bandari hizo ili kuharakisha maendeleo ya nchi yetu,” alisema Mwanri.

Pamoja na hayo, Mwari alitembelea maeneo ya Bandari ya Tanga na kushuhudia shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati namba 2 ikiwa ni moja ya malengo katika kuimarisha huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini hapo. 
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua ukarabati wa boti katika Bandari ya Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...