Na: Genofeva Matemu – WHUSM,

Wadau wa Tasnia ya Filamu na Muziki wameishauri Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) kuandaa upya mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa kuwa na takwimu kutoka kwa Taasisi zote zinasimamia sekta ya Filamu na Muziki nchini.

Rai hiyo imetolewa na wadau mbalimbali wa tasnia hizo walioshiriki katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwasilisha mwongozo huo kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa ni vyema mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kutoka TCDB kuzingatia takwimu na taarifa sahihi kutoka kwa wadau ili kuweza kuendana na hali halisi ya tasnia hizo.

“Katika kutekeleza azma ya Taasisi ya TCDB ni vyema mkaandaa mchakato wa kufikia na kushirikisha vyombo vya wadau kuanziia ngazi ya chini kwa kupitia shirikisho la filamu pamoja na Taasisi za Serikali ambao watachangia katika kuandaa mwongozo ulio bora” amesema Bw. Mwakifwamba.

Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu (kushoto) akielezea mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii wakati wa kikao na wadau wa tasnia ya Filamu na Muziki leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo 
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akizungumza na  wadau walioshiriki katika kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu. 
Mjumbe kutoka COSOTA Bw. Paul Makula akichangia mada wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...