Beki wa kulia na nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil kwenye Kombe la Dunia Mwaka 1970  Carlos Alberto amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72,  klabu yake ya zamani Santos imetangaza leo.
Beki huyo amechezea Brazil mara 53 na kufunga goli linalotajwa kuwa bora zaidi katika historia ya Kombe la Dunia kwa kupiga shuti kali lililomaliozia ushidni wa bao 4-1 dhidi ya Italy kwenye fainali hizo za mwaka 1970 (angalia video hapo juu).
Kwa mujibu wa habari kutoka Brazil Carlos Alberto alifariki kwa ugonjwa wa moyo. Alipata kuchezea vilabu vya  Fluminense, Santos, Flamengo na New York Cosmos kati ya miaka 1962 hadi  1982 kabla ya kuwa kocha.Taarifa ya klabu ya Santos imesema: "Carlos amecheza jumla ya mechi 445  na kufunga magoli 40 goals toka 1965-1975, na anasifika kuwa beki wa kulia bora kabisa katika Brazil". Klabu hiyo imetangaza siku tatu za maombolezo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...