Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii Buhigwe-Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti amezindua ujenzi wa madarasa 276 ya shule za msingi Wilayani Buhigwe ilikuhakikisha wanamaliza kero ya upungufu wa madarasa katika wilaya hiyo ambayo yatakamilika kwa Kipindi cha Mwaka mmoja ili kumaliza kero ya muda mrefu. 

Akizungumza na Wananchi wa wilaya Hiyo katika uzinduzi wa Ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika kijiji cha Mnyegera aliwaomba Wananchi Kumuunga mkono ilikuhakikisha Wanamaliza tatizo hilo na watoto wanasoma Katika Mazingira mazuri na kupata elimu nzuri itakayo wasaidia kuepukana na umasikini.

Gaguti alisema Baada ya kuona hali ya ukosefu wa madarasa katika Wilaya hiyo inayopelekea Wanafunzi kukosa vyumba vya kusomea kutokana na wingi wao aliamua kuweka kambi katika kila Kata kujenga shule mbili ambapo anatarajia kujenga shule 276 kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo ilikuepukana na upungufu wa Vyumba vya madarasa.

" Baada ya kuona takwimu na kujionea hali halisi ya Shule Zetu nilitambua nilazima tuchukue Jukumu la kubadili hali hii nitaweka Kambi Kila Kata kuhakikisha Jukumu hili linakamilishwa Ndani ya Muda tuliojipangia,pia ni washukuru Wananchi na viongozi kwa muitikikio na Dhamira ya kushirikiana na Serikali kuniresha miundo mbinu ya Elimu",alisema Gaguti.

Nae Afisa Elimu wa Halmashauri ya Buhigwe ,Deo Fande alisema Halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa Vyumba vya Madarasa 672 kutoka na Elimu kutolewa bute wazazi wengi wameleta watoto wao iliwaweze kupata elimu hiyo hali iliyo pelekea upungufu wa madarasa.

Fande alimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutoa kipaumbele cha kujenga madarasa na aliwaomba Wananchi kuendelea kujitoa kwa Wingi kuchangia kujenga madarasa yatakayo kuwa hayakujengwa na Wilaya na kushirikiana na viongozi kujenga madarasa hayo.

Kwa upande wao Wananchi Wa Wilaya ya Buhigwe ,Pelesi Makaya na Abasi Mvuyekule walisema wanampongeza Mkuu wa Wilaya kwa kujitoa kushirikiana na Wananchi kwa kuwasaidia watoto wao kuepukana na mazingira magumu ya kusomea iliyo kuwa ikiwatesa watoto hao.

Aidha Wananchi hao wamemuahidi Mkuu wa Wilaya kushirikiana nae kwa kuchangia maendeleo na kuwawezesha Watoto kukaa na kupata madarasa mazuri yatakayo pelekea watoto kupata elimu iliyo bora na itakayo wasaidia katika maisha yao.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti akitoa maelekezo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa madarasa 276 ya shule za msingi Wilayani Buhigwe .
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buhigwe Elisha Bagwinya,wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa madarasa 276 ya shule za msingi Wilayani Buhigwe . 
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti akishiriki ujenzi wa moja ya madarasa sambamba na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buhigwe Elisha Bagwinya,mara baada ya kuzinduliwa kwa ujenzi wa madarasa 276 ya shule za msingi Wilayani Buhigwe .Picha na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...