Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa   Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 26, 2016. 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. usimtafute mchawi nd rais , hii yote ni watu kuajiriana kindugu / kirafiki/kikabila /kidini na kujuana bila kujali uwezo na ujuzi wa anayeajiriwa, hao wote inaonyesha hawajui wanachikifanya katika kazi zao

    ReplyDelete
  2. Jamani, Mbona hawa watu wanafanya upuuzi sana bandarini? Wanafanya kazi kana kwamba ni watoto/wajinga. Systems zao hazifanyi kazi. Ni rahisi sana kwa watu kuiba au kupitisha chochote bila wao hata kujua chochote.

    ReplyDelete
  3. Hii kali. Kweli kuna mwendo.
    Msemaji hapo juu umesema kweli

    ReplyDelete
  4. Hongera Mheshimiwa Rais. Kila Mfanyakazi lazima awe na Mafunzo halali na uajiri ufuate uwezo wa utendaji kutokana na Elimu Husika. Kwa vile kuna Wenye vyeti halali ila hawana uwezo wa kufanya kazi kivitendo.

    ReplyDelete
  5. duhhh kazi kweli kweli, nahisi hapo mjibu maswali alikuwa anatetemekea miguu..hadi mdomo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...