Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mh Abdallah Hamisi Ulega

 Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt, Nassoro Ally Hamidi akila kiapo
Mkuu wa Wilaya ya  Ruangwa Mh Agnes Elias Hokororo  akipokea nyenzo za kufanyia kazi
  Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh  Regina Reginal Chonjo akila kiapo
MKUU wa mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo, kufanya kazi waliyokabidhiwa ikiwemo kuwatumikia wananchi katika maeneo yao kwa kufuata kanunu na maadili kwa kushirikiana na jamii ili kuwaletea maendeleo kutokana na hali duni za wananchi wa mkoa wa Lindi wenye raslimali nyingi.


Wito huo umetolewa na Muda mfupi baada ya kuapishwa wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Lindi ambapo aliwahimiza kufuata kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali zilizowekwa na Serikali, kwani ndio misingi mikuu
itakayowasaidia kutekeleza vema majukumu yao ya kila siku katika wilaya zao.



Aidha alisisitiza wakuu hao kusimamia na kufuatilia miradi inayotekelezwa katika wilaya zao,pamoja na kuzingatia fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wake inalingana thamani halisi ya fedha inayotolewa (Value for money).



Mara baada ya kuapishwa mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Hamisi Ulega alieleza kuwa kwa nafasi yake atatekeleza vema maamuzi ya vikao vya serikali na kusimamia hasa maamuzi ya Kamati ya Ushauri mkoa (RCC)kuhusiana na ununuzi wa zao la ufuta linalozalishwa kwa wingi wilayani kwake.



Nae mkuu wa wilaya ya Nachingwea Regina Reginal Chonjo,Licha ya kushukuru kwa kuteuliwa Mkuu wa wilaya hiyo alihaidi kushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo ambao tayari wamemwonyesha njia baada ya wananchi hao kujitolea kujenga jingo la ofisi ya mkuu wa wilaya na Halmashauri yao.



Wakuu walioapishwa ni Dkt, Nassoro Ally Hamidi,aliyepangiwa wilaya ya Lindi, Abdallah Hamisi Ulega (DC,Kilwa),Regina Reginal Chonjo (DC Nachingwea),Agnes Elias Hokororo (DC Ruangwa) na Ephem Mbigi Mmbaga (DC Liwale). Picha na Habari toka kwa mdau Abdulaziz Video -Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...