Wanafunzi na walimu kutoka nchini uholanzi wakikabidhi vifaa vya maabara kwa shule ya sekondari ya Oltinga ambayo ni ya kata ya selala wilayani Monduli.anayeshuhudia aliyevaa suti nyeusi ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Mh Edward Sapunyu
 Wanafunzi wa uholanzi wakitoa msaada wa  laptop kwa wana jumuia ya shule ya sekondari ya Oltinga ambayo ni ya kata ya Selela wilayani Monduli.
 Sehemu ya wanafunzi wa Uholanzi wakifuatilia shughuli za hutoaji wa misaada ya vifaa vya maabara na  laptop kwa shule ya sekondari ya Oltinga iliyopo Monduli
 sehemu ya wanafunzi kutoka Uholanzi katika hafla hiyo
Baadhi ya wanakiji wa jamii ya kabila la wamasai wakifuatilia upokeaji wa misaada ya vifaa vya maabara na laptop kutoka kwa wanafunzi wa Uholanzi.

Habari na picha na  
Novatus Makunga.
Shule ya sekondari ya kata ya jamii ya wafugaji wa Kimaasai ya Oltinga iliyopo Monduli mkoani Arusha imepata vifaa vya maabara na kompyuta ndogo aina ya laptop kumi na tano vilizotolewa na kundi la wanafunzi na walimu kutoka nchini Uholanzi


Wafadhili hao pia limeahidi kugharamia nusu ya fedha ya uwekaji wa umeme wa nishati ya jua yaani solar power

Wanafunzi hao kumi na wawili na walimu wao wanne wamekabidhi msaada huo katika shule hiyo iliyopo katika kata ya selela ambapo kiongozi wao Marianna Groenewoud ameeleza kuwa wataisaidia shule hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu

Makamu mkuu wa shule hiyo John Masoi ameiomba serikali kusaidia kutoa kiasi kilichobaki cha gharama ya uwekaji wa umeme wa nguvu ya jua unaohitaji jumla ya shilingi milioni kumi na mbili

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Edward Sapunyu ameeleza kupitia wakala wa nishati vijijini[rea],halmashari hiyo itaweka umeme katika sekondari hiyo

Mratibu wa misaada hiyo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya stichting tanzania support Melchior Nguma ameeleza mbali ya shule hiyo pia wamesaidia shule ya msingi na zahanati ya kijiji cha selela



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...