THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

There was an error in this gadget

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 8, 2016


News Alert: Rais Magufuli afanya mabadiliko ya Makatibu wakuu, Naibu Katibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;
Dkt. Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. Dkt. Maria Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.Bw. Christopher Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Dkt. Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina. 

Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya 
Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

07 Desemba, 2016


RC MAKONDA AWAKARIBISHA WANA DAR ES SALAAM NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU


Rais Mstaafu Jakaya Kikwete afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia

Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) juzi tarehe 6 Desemba, 2016, amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Haile Mariam Desale alipomtembelea ofisini kwake jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi Waziri Mkuu wa Ethiopia Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanaopata elimu iliyo bora na kwa kiwango kinachofanana dunia nzima.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea.

Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufikida pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo.

Rais Mstaafu ameiomba Ethiopia kujiunga na Mpango huo ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia ameelezea nia ya nchi yake kujiunga na Mpango huo. Ethiopia ni moja kati ya nchi za Afrika ambayo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa fursa ya elimu kwa watoto na vijana wake. Pamoja na mafanikio makubwa bado zipo changamoto zinazohitaji hatua madhubuti ili kufikia lengo la kizazi cha elimu ifikapo 2040.

Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda na Malawi na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis Ababa.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkabidhi Ripoti ya Kamisheni ya Elimu Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desale jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia.


JARIDA LA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) - ONLINE EDITIONRAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana tarehe 07 Desemba Ikulu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU


ANDIKA NA SOMA : shindano la uandishi wa hadithi fupi kwa wanafunzi wa sekondari nchini

Tunapokea hadithi fupi yenye maneno yasiyopungua #1000 wala kuzidi #3000. Dhamira ni #Utandawazi.
Vigezo: Tumia lugha nyepesi, fasaha, yenye visa, wahusika na vionjo vya kisanii kuandika hadithi fupi. Zingatia jinsia na kuonesha badala ya kuhubiri. Si lazima utumie neno‘UTANDAWAZI’ katika hadithi yako.Mwisho wa kupokea hadithi ni tarehe 28 February 2017. Zawadi nono zitatolewa kwa washindi ikiwa ni pamoja na kuhudhuria warsha ya mafunzo ya uandishi.
 ANDIKA NA SOMA ni shindano la fasihi linalohusisha wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania.

Shindano linadhamiria kuwapatia fursa vijana kushiriki mijadala ya kijamii kwa kutumia fasihi. Vivyohivyo, kupitia shindano hili tunawajengea ari na stadi zitakazowawezesha kuwa wasomaji mahiri na wachambuzi wa mambo anuwai katika jamii; pamoja na kuimarisha uwezo wao wa kuwasilisha fikra zao kwa ufasaha na wabunifu.


Afrika ijifunze kutoka Korea, Mawaziri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba ya Tanzania kwenye Mkutano wa Nne wa Ushirikiano wa nchi za Afrika na Jamhuri ya Korea uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba 2016.
Mhe. Waziri Mahiga akipitia makabrasha ya mkutano. Nyuma ya Mhe. Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika, Mhe. Naimi Aziz na Afisa wa Ubalozi huo, Bi Suma Mwakyusa.
Habari kamili BOFYA HAPA


GOLOLI ZATUMIKA KUPIGIA KURA UCHAGUZI WA GAMBIA

Inline image 4Huenda Jambo Kubwa sana ulilojua kuhusu uchaguzi wa Gambia ni Kuondolewa kwa kiongozi nguli wa Nchi Hiyo Yahya Jameh na sana kama unafuatlia medani za siasa katika duru la Kimataifa utagundua pia kwamba Gambia ilikataa katu kuruhusu waangalizi wa umoja wa Ulaya bila kutoa sababu zozote....hata hivyo Waangalizi kutoka Muungano wa Afrika (AU), Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya mataifa ya kiislamu OIC waliruhusiwa.

UCHAGUZI wa Taifa dogo la Afrika Magharibi la Gambia lililopo kilometa chache ukingoni mwa Jangwa la Sahara, uligubikwa na mvuto wa kipekee kutokana na wasifu wa wagombea wawili waliochuana vikali. Rais aliyebwagwa katika uchaguzi huo, Yahya Jammeh, aliyetawala kwa miongo miwili na ushei aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi ya kijeshi amekubali kushindwa na kuahidi kukabidhi madaraka kwa amani kwa mpinzani wake aliyeshinda, Adama Barrow, ambaye hajawahi kuongoza katika ngazi yoyote ya kisiasa.
Wagombea wote wawili wanawiana kwa umri (miaka 51) ambapo Jammeh aliyeingia madarakani kwa Mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu mwaka 1994 alijipatia asilimia 36 ya kura zote zilizopigwa, Barrow alijipatia asilimia 45 na mgombea wa tatu Kandeh alijipatia asilimia 17.8.

 Pengine matokeo hayo yaliyopokewa kwa nderemo na vifijo si kivutio kikubwa zaidi cha uchaguzi, lakini ni mfumo mbadala wa Taifa hilo katika kupiga kura unaotofautiana na mataifa mengine kwa kutotumia kadi za kupiga kura bali kinachotumika ni gololi zisizokuwa na rangi wanazotumbukiza wapiga kura katika pipa lenye rangi inayomwakilisha mgombea wanayetaka kumchagua.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA


NGOMA AZIPENDAZO ANKAL - Darassa ft Ben Pol - Muziki


RAIS WA UFARANSA AFUNGUA MKUTANO WA 4 WA OGP,MKURUGENZI TWAWEZA AELEZA MUELEKEO

 Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande akihutubia washiriki katika ufunguzi wa mkutano wa 4 wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP) katika ukumbi wa Salle Pleyel, ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwataka washiriki kuja na matokeo ya hatua zilizochukuliwa katika kushirikisha wananchi kwenye masuala ya maendeleo.
Washiriki wakimsikiliza Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande
 Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza Bw.Aidan Eyakuze (kulia) akishiriki katika majadiliano wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 4 wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP) katika ukumbi wa Salle Pleyel,ambapo walijadili masuala mbalimbali ya Serikali kwa uwazi nakueleza mtazamo wake juu muelekeo wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP).


MUZIKI WA DARASSA WAPAGAWISHA WANA-MBEYA


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


Kilimanjaro International Airport (KIA) update


VIKWAZO VISIVYO VYA KIKODI KATI YA TANZANIA NA RWANDA VYATAKIWA KUONDOLEWA KATIKA KUKUZA BIASHARA

Picha ya pamoja ya viongozi waandamizi kati ya Tanzania pamoja na wafanya biashara wa Rwanda.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ni wa kimaendeleo hivyo lazima kuondolewa kwa vikwanzo visivyo vya kikodi.

Ngonyani ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa siku mbili kati Tanzania na Rwanda kujadili masuala ya maendeleo ya biashara kati ya nchi hizo, amesema kuondolewa kwa vikwanzo visivyo vya kikodi kutaongeza maendeleo katika nchi zote mbili katika ukuaji wa uchumi.

Amesema bidhaa zinazozalishwa nchini  Tanzania  zikifika Rwanda ziweze kukubalika hivyo hivyo na bidhaa za Rwanda zikubalike na mamlaka zilizopo hapa nchini.

Ngonyani amesema Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji ambapo wananachi wa Rwanda wanaweza kuwekeza  hapa nchini .

Naye Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki wa nchini Rwanda, Francois Kanimba amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania ni maendeleo ya kibiashara katika sekta mbalimbali ikiwemo ya sekta ya usafirishaji.

Aidha amesema  mkutano huo utatoa matumaini mapya kwa nchi hizi mbili kuweza kunufaika na kibiashara pamoja na  kutatua changamoto  wanazozipata wafanyabiashara wa nchi hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano, Mh. Edwin Ngonyani akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika mkutano kujadili masuala ya biashara kati ya Tanzania na Rwanda leo jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mamlaka za Rwanda na Tanzania pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania.

Viongozi wa waandamizi wa Tanzania na Rwanda wakitembeleo baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini na Kampuni ya Rwanda leo jijini Dar es Salaam.


YALE YALEEEE.......

 Mtembea kwa miguu ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiwa amesimama katikati ya barabara kutaka kuvuka katika eneo lisilokuwa na alama za kivuko, huku magari yakiendelea kupita kwa kumkwepa, katika Barabara ya Kigogo Jijini Dar es salaam.


WABUNIFU WA BIDHAA ZA KILIMO WAKUTANISHWA NA TASISI ZA FEDHA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Jumla ya Vikundi 16 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini vinavyojihusisha na masuala ya kilimo vimekutanishwa na Tasisi za kifedha na mabenki ili kuwezeshwa kama mpango wa taasisi ya Land O Lakes.

Akizungumza na Globu ja Jamii,Mshauri wa biashara bunifu kutoka tasisi hiyo ,Renalda Lema amesema kuwa katika vikundi hivyo 16 wamewakilishwa na watu wawili wawili,ili kuwasilisha ubunifu wao kwa taasisi hizo na kupata fursa ya kupanua biashara yao.

“Kama ambavyo unaweza kuona wabunifu walivyotengeza mashine mbalimbali, ambazo zitaweza kumuondoa mkulima kutoka sehemu moja hadi nyingine, hasa katika serikali hii ambayo inahamasisha uchumi wa viwanda, hivyo sisi tumeona uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa bila ya kuanza kuwawezesha wakulima katika hatua ya awali kabisa” amesema Renalda.

Ametoa wito kwa wadau na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kuwawezesha wakulima hao kwa namna moja ama nyingine,kuwasiliana na taasisi ya Land O’ Lakes kuwakutanisha na wakulima hao.
Mkurugenzi wa tasisi ya fedha ya Brac, Mahufuzii Ashrafu , akizungumza na baadhi ya wabunifu waliokutanishwa na kampuni hiyo ili waweze kuwezeshwa kama mpango wa tasisi ya Land O Lakes ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Mbunifu wa mashine ya kukamua matunda kutoka mkoa wa Songwe, Yohana Mwanzyunga(wa kwanza kulia) akiwaonyesha washiriki wengine mtambo wa kukamua matunda.
Baadhi ya washiriki wakiangalia mashine ya kupukucha halizeti


MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA USAFIRI WA ANGA DUNIANI(ICAD

 Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari za jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Vallery Chamulungu wakati akiongea na kuzindua Kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku Usafiri wa anga Duniani(ICAD) yaliyofanyika makao makuu ya (TCAA) Ukonga Banana jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la kongamano hilo ilikuwa ni kuwahamasisha wanafunzi hao wapende masomo yanayohusiana na usafiri wa Anga.
 Afisa mwanadamizi Idara ya uongozaji ndege Mwanajumaa Kombo  akitoa elimu juu ya masuala ya uongozaji wa ndege  kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari za jijini Dar es Salaam,  wakati wa Kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku Usafiri wa anga Duniani(ICAD), yaliyofanyika makao makuu ya (TCAA) Ukonga Banana jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la kongamano hilo ilikuwa ni kuwahamasisha wanafunzi hao wapende masomo yanayohusiana na usafiri wa Anga.
 Mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania Aristid Kanje akitoa mafunzo juu ya kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo cha Usafiri wa Anga(CATC),wakati Kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku Usafiri wa anga Duniani yaliyofanyika makao makuu ya (TCAA) Ukonga Banana jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la kongamano hilo ilikuwa ni kuwahamasisha wanafunzi hao wapende masomo yanayohusiana na usafiri wa Anga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


BIDHAA ZA MCHELE NA CHUMVI ZAENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE


MAJALIWA AKITAZAMA GARI LILILOJENGEWA BODI LA MBAO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama gari aina ya Toyota iloyojengewa bodi la mbao wakati alipotembelea kiwanda cha Fibreboars 2000 Limited cha Arusha akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo Desemba 5, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


UKOSEFU WA HUDUMA YA KWANZA KWENYE VIWANJA MIKOANI KUNAWEZA KULETA MAAFA MAKUBWA

Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BAADA ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4, Hospitali wametoa ripoti ya kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Mwadui FC.


 Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi, Ismail alifariki uwanjani kutokana na kupata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (Sudden Cardiac Arrest-SCA).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote ila baada ya uchunguzi walibaini kusimama ghafla kwa moyo (Sudden Cardiac Arrest) kulisababisha kifo.

Kulifunguliwa jalada la uchunguzi, bahati nzuri madaktari walifanya huduma ya haraka, kwa mwonekano huyu marehemu Ismail Mrisho Khalfan ambaye ndiye alikuwa ameanguka pale uwanjani kwa nje hakuonekana kuwa na jeraha kwa hiyo madaktari wakatueleza lazima afanyiwe uchunguzi wa kina.

Kutokana na tatizo hilo, Ismail alitakiwa kupatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuanguka kwa kupata msaada ni kupata electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache baada ya kubainika kuanguka na ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache.

Kitaalamu kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.


Ukosefu wa vifaa uwanjani ikiwemo daktari mkuu wa uwanja na gari la wagonjwa limekuwa kama wimbo wa taifa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwa kushindwa kuwa na vifaa hivyo na pale mchezaji anapotokea anapata tatizo anashindwa kupata huduma kwa usahihi na wakati muafaka ,na ikumbukwe katika msimu huu wa ligi kuu Vodacom, Golikipa wa timu ya African Lyon aliweza kuvunjika mbavu katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu lakini hakukuwa na gari ya wagonjwa na aliishia kubebwa kwenye gari aina ya Pick up.

Tumeshuhudia mchezaji wa Stand United Chidiebele akiumia uwanjani na kuvunjika taya lakini hakukuw ana huduma ya uhakika achilia hao wapo wachezaji wengi wanaopata madhara ila uhakika wa huduma katika viwanja vya mikoani ni mdogo sana na hata katika ripoti za waamuzi wamekuwa wakiandika kutokuwepo kwa gari la wagonjwa ila hakuna jitihada zinazofanywa.


MAJENERALI WAPYA WAVISHWA VYEO MAKAO MAKUU JWTZMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (Kushoto), akimvisha cheo cha Meja Jenerali,Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali George William Ingram,Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) akimvisha cheo cha Meja Jenerali Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo, Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (Wa pili kushoto) pamoja na mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salvatory Mabeyo (Wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na ma Meja Jenerali wapya, Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.

Picha kwa hisani ya kurugenzi ya habari na uhusiano JWTZ


TAARIFA KWA UMMADKT. SHEIN MGENI RASMI MAHFALI YA 14 CHUO KIKUU CHA TUNGUU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa mgeni rasmi katika Mahfali ya Kumi na Nnne yaliyofanyika Chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal alipokuwa akiwatunuku Stashahad na Shada wahitimu katika fani mbali mbali wa mwaka 2016 wakati wa sherehe ya Mahfali ya kumi na nne yaliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi kutoka wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal wakati wa sherehe ya Mahfali ya kumi na nne iliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe ya mahfali ya kumi na nne (14) katika Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kulia) Prof.Saleh Idriss Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo na (kushoto) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal.


SAANYA, MPENZU, MROPE WAONDOLEWA KWENYE RATIBA YA LIGI KUU


WAAMUZI waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.

Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia daraja lengine la uamuzi.

Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.

Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake.

Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo kumalizika kwa vurugu. 

Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.

kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.


Wateja 15,345 wafaidika na Mradi wa Umeme wa KIA

Na Teresia Mhagama
Imeelezwa kuwa zaidi ya wateja wa awali 15,345 wameunganishwa na huduma ya umeme baada ya kukamilika kwa mradi wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kituo hicho.

Dkt. Pallangyo alisema kuwa, mradi huo ulihusisha ujenzi wa Transfoma mbili zenye uwezo wa Megawati 20 kila moja (2x20MVA) pamoja na jengo la kuendeshea mitambo ambapo Kituo kinasambaza umeme kwa wateja kupitia njia 6 za msongo wa kilovoti 33.

“Niseme tu kuwa, mradi huu ni muhimu sana kwani kukamilika kwake kumeboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Wilaya ya Hai, migodi ya Mirerani na maeneo mengine ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha,” alisema Dkt. Pallangyo.

Aliongeza kuwa Kukamilika kwa kituo hicho kumeimarisha pia upatikanaji wa umeme katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Alisema kuwa, utekelezaji wa Mradi huo ulianza rasmi tarehe 22 Machi, 2010 na gharama za mradi ni Shilingi bilioni 15.3 sawa na Dola za Marekani milioni 7.08.

Mradi huo wa KIA umetekelezwa kupitia Mradi wa TEDAP ulio chini ya Wizara ya Nishati na Madini ambao unahusika na uboreshaji wa njia za usafirishaji, usambazaji na ujenzi wa vituo vya umeme katika Mikoa ya Dar es salaam, Arusha na Kilimanjaro. 

Mradi wa TEDAP unahusisha Ujenzi wa njia za kusafirishia umeme wa msongo wa kilovolti 132, ujenzi wa vituo vitano vya kupozea umeme jijini Dar es salaam pamoja na Kituo cha kupozea Umeme cha KIA.

Mradi pia unahusisha ujenzi wa vituo vipya 19 vya kusambaza umeme wa msongo wa kilovolti 33 pamoja na njia za usambazaji umeme kwa urefu wa kilomita 102.497 za msongo wa kilovolti 33 na kilomita 34.018 za msongo wa kilovolti 11 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro.
 Naibu Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akikagua Chumba cha kuongozea Mitambo ya Umeme kwenye Kituo cha kupoozea  Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.  Kulia ni Mhandisi Neema Rushema, Mhandisi Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
 Naibu Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akikagua Mitambo ya Umeme kwenye Kituo cha kupoozea Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.  Kushoto Mhandisi Neema Rushema, Mhandisi Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini.


Baadhi ya mitambo ya Umeme katika Kituo cha Kupoozea Umeme cha KIA.


KATIBU MKUU WA TIMU YA RYHNO RANGERS AFUNGIWA MIEZI MITATU

KATIBU Mku wa klabu ya Rhino Rangers, Dickson Cyprian Mgalike amefungiuwa miezi mitatu kwa kosa la kuidanganya kamati kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia Bodi ya Ligi.

Maamuzi hayo yametolwa na Kamati ya usimamizi na uendeshaji baada ya kupitia ripoti nzima na kugundua kuwa Mgalike aliwadanganya na imeamua kumpa adhabu ya Kumfungiwa miezi mitatu.Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.

Katibu aliandika barua kusema kwamba Sameer hakufanya kosa hilo na alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kufuata kanuni ya 41(6).


SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA YA AFYA WALEMAVU WA NGOZI

Na Anthony John Globu ya Jamii.


CHAMA cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimetoa wito kwa Serikali kuwapatia bima ya Afya watu wenye ulemavu wa ngozi ili kuweza kuwasaidia pale wanapokuwa na matatizo ya kiafya.

Akiongea  na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam katika Ofisi ya chama hicho iliyopo hospitali ya Ocean Road, Muweka hazina Abdilah Omary amesema watu wenye ualbino hasa waliopo vijijini wanapata changamoto kubwa ya upatikanaji wa matibabu hasa pale wanapo sumbuliwa na magonjwa mbali mbali.

 Abdilah ametoa wito kwa jamii na familia zenye watu wenye ualbino kuwapa malezi yanayoendana na hali yao tofauti na Jamii nyingi kwa hivi sasa wanawalazimisha watu wenye ualbino kufanya kazi ngumu kama kuchunga ngo'mbe na kulima.

Wakati huo huo wajumbe wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania wamemchangia kiasi cha sh.milioni moja Leonard Gaspar mwenye ulemavu wa ngozi Mkazi wa Morogoro Matombo anayesumbuliwa na kansa ya ngozi.

Hata hivyo Leonard  amewashukuru wajumbe wa chama hicho kwa mchango huo huku akiomba jamii na wadau mbalimbali kuwapa msaada pale wanapoweza ili apate mtaji wakumsaidia katika maisha ya kila siku na matibabu.

Chama hicho cha watu wenye ualbino Tanzania wametoa wito kwa jamii kumsaidia kijana Leonard anaye sumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi kwa muda mrefu.

Hata Hivyo Abdilah ameomba Jamii ya watanzania watakaoguswa na tatizo alilonalo Leonard wanaweza kutoa michango yao kwa kuwasiliana na Ofisi za Chama Cha Watu Wenye Ualbino kilichopo Katika Hospital ya Ocean Road.


Muweka hazina wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania, Abdilah Omari  akiwa pamoja Leonard Gasper anayesumbuliwa na tatizo la kansa na kumpatia msaada wa kiasi cha fedha milioni moja kwa ajili ya matibabu.


WAHARIRI WAKUTANA KUPITIA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI ILIYOPITISHWA NA BUNGE

Na Dotto Mwaibale.

WAHARIRI wa vyombo vya habari wamekutana katika mkutano maalumu wa siku mbili kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa yanayohusu tasnia hiyo nchini.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga alisema mkutano huo utawajumuisha wadau wa sekta ya habari kutoka ndani na nje ya nchi.

"Tumewaalika wenzetu wa nje ili watupe uzoefu wa jinsi wanavyofanya katika tasnia ya habari katika nchi zao" alisema Makunga.

Alisema katika mkutano huo ambao unafanyika Hoteli ya Protea Court Yard mambo yatakayo zungumziwa ni kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na kujadili mpango mkakati wa Jukwa la Wahariri wa kuendeleza tasnia ya habari nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura alisema ni muhimu kwa wanahabari kuwa na mpango mkakati wa miaka 10 ili kupata majibu sahihi ya tasnia hiyo.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri  kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
 Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile akizungumza kwenye mkutano huo.
 Taswira ndani ya ukumbi wa mkutano huo
Wahariri ndani ya chumba cha mkutano.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


WANANCHI WA SINGIDA KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA UPEPO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mh. January Makamba amesema kuwa mpango wa serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji umeme ili kuwa na vyanzo vya nchi endelevu na kuunga mkono juhudi za benki ya dunia kuzalisha umeme wa upepo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Makamba amesema hayo wakati wa Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme walipokutana kuzungumzia matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa njia ya upepo itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo utawasaidia wananchi wa Singida .

"Kwa kuwa umeme huo utazalishwa kwenye maeneo ya vijijini, wananchi wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi kulingana na uchumi wao na sio kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi Wizara yake inapenda kuweka  wazi kuwa huu mradi una faida kubwa sana kulingana na mfumo wa nchi ulivyo,"amesema Makamba.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six Telecoms,  Rashid Shamte amessema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una faida kubwa sana kwa wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti ya benki ya dunia wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali imekubaliana na kampuni yetu na  imeweza kukubali kuwa mradi huu una  tija na  utasimamiwa na serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na Halmashauri.

Shamte ameendelea na kusema, kwa Phase ya kwanza watatoa umeme megawati 100 na itaendelea mpaka kufika megawati 300 na wataunganisha kwenye gridi ya taifa, na huu mradi utakuwa na faida kwa wananchi pamoja na wale watakaotolewa kwenye maeneo yao watafaidika kwa kulipa stahiki zao.

Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amewataka wawekezaji hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi mipango ya serikali imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo wanategemea kuona kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini kupata umeme kwa bei rahisi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa umeme kujadili mkakati ya kuzalisha nishati ya Umeme kwa njia ya Upepo leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Jijini Dar.